Album mpya ya Solange yashika namba moja kwenye chati za Billboard 200, rekodi aliyoweka na Beyonce iko hapa..

Album mpya ya dada yake Beyonce ‘Solange‘ imeshika namba moja kwenye albuum zenye mauzo makubwa zaidi wiki hii kwenye chati za Billboard top 200.
Album inaitwa ‘A Seat at the Table‘ imeuza nakala 72,000 (kwa ununuzi wa kidijitali ‘OnLine Sales’ ) katika wiki yake ya kwanza kwa mujibu wa Nielsen Sound Scan.
Album hiyo ilitoka chini ya label yake mwenyewe iliyopewa jina Saint Records kwa ushirikiano wa Columbia Records. Cd za album zinatoka November 18 2016.
REKIDO>>Solange na Beyonce wameweka rekodi ya kuwa ndugu waliowahi kushika namba moja kwenye chati hizo na kujiunga kwenye rekodi hio na wasanii kama Michael Jackson na Janet Jackson, Master P na kaka yake, Silkk the Shocker.
#StoriBy Mellisa


EmoticonEmoticon