
Mwaka 2015 producer mkongwe na maarufu duniani Dr. Dre aliomba msamaha wanawake wote aliowahi kuwanyanyasa kwenye mahusiano yao alivyokuwa kijana.
Msamaha huo aliutoa baada ya mwandishi wa habari Dee Barnes kuweka wazi baadhi ya matendo ya unyanyasaji aliyoyafanya Dr Dre mwaka 1991.
Dre alimuomba msamaha aliyekuwa mpenzi wake Michel’le ambaye yeye anasema alivimbishwa macho kwa ngumi zaidi ya mara tano na kuvunjwa mbavu.
Baada ya Miche’le na stori yake kukwepwa kwenye filamu ya N.W.A. ya Straight Outta Compton, Michel’le anatoa filamu fupi itakayoongelea maisha yake na inasemekana patakuwa na matendo ya unyanyasaji yaliyofanywa na Dr Dre na Producer huyu anampango wa kufungua kesi dhidi ya Michel’le kama mambo hayo yataonyeshwa.
Filama Ya Michel’le inaitwa Surviving Compton: Dre, Suge & Michel’le na itatoka October 15.
Kwa mujibu wa TMZ, picha hii itaonyesha Dr Dre akimpiga Michel’le, kumvuta nywele na hata kumtishia silaha ya moto.
Dr Dre anasema hakuwahi kumpiga Michel’le walivyokuwa pamoja miaka 30 iliyopita na kwamba atafungua kesi dhidi ya watayarishaji wa filamu hio sababu hapakuwa na kithibitisho chochote kutoka hospitalini au polisi kilichosema mambo hayo yametokea.
#StoriBy Mellisa
EmoticonEmoticon