Leo October 31 2016 aliyekua Miss Tanzania 2004 Faraja Kotta Nyalandu ametumia ukurasa wake wa Intagram kumuandikia ujumbe wa kumtia moyo na kukumbushia ilivyokua kwake baada ya kutangazwa mshindi mwaka 2004.

‘Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda, asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya shindano. nilipigiwa simu kuamshwa, nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani. Nilitetemeka‘
‘Nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia. niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili, nilijuta kushiriki Miss Tanzania… nilikua mdogo na sina uelewa wa mambo mengi, ndio nilikua nimefikisha umri wa miaka 19, na hapo tu ndio natoka shule ya boarding tena ya Katoliki’ sikujua kuna watu wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua’ – Faraja Nyalandu

‘Iliwibidi wazazi wangu ambao wameshafariki (RIP) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie vizuri, haikua rahisi… nilijifunza na leo hii hakuna binadamu mwenye hiyo nguvu niliyompa yule mtangazaji… nilijifunza kupitia mabaya na nashukuru kwa fundisho hilo’ – Faraja
Kwa kumalizia Faraja ameandika ‘Namshukuru Mungu nilijifunza mapema, kuna sehemu ya nguvu niliyonayo leo iliyotokana na kujeruhiwa na binadamu na kupona lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona, unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja, usijitafutie laana za rejareja… sasa kwa Miss Tanzania mpya uliyechaguliwa, fanya yako… wengine tuliobaki tujenge zaidi ya kubomoa. upendo haugharimu chochote‘
A photo posted by Faraja Nyalandu (@farajanyalandu) on Oct 30, 2016 at 10:18pm
EmoticonEmoticon