Man United wajipooza machungu kwa Rojo baada ya kutolewa UEFA

Baada ya kutolewa na Sevilla katika hatua ya kutinga robo fainali ya Uefa, Manchester nited wamejipooza kwa kumuongezea mkataba beki wao kisiki raia wa Argentina, Marcos Rojo.
Man United wamempa mchezaji huyo mkataba wa miaka mitatu na nusu ambao utamuweka kwenye timu hiyo hadi Juni 2021.
“Baada ya kusaini mkataba huo Rojo amesema, “Ninafurahi sana kusaini mkataba mpya Manchester United. Tangu nilipojiunga na Manchester United nimejifunza kila kitu na zaidi,” amesema Rojo.
“Nina furaha sana kuendelea kukaa kwangu katika klabu hii kubwa. Nilipojiunga lengo langu ni kusaidia timu kushinda mataji na tumefanya hivyo misimu iliyopita. Ninafanya kazi kwa bidii kurudi uwanjani. Ningependa kuwashukuru mashabiki kwa msaada wao na kocha kwa kunisaidia kunipa ujasiri ndani na nje ya uwanja,” ameongeza.
Man United Jumamosi hii itakuwa katika uwanja wake wa Old Trafor kucheza na Brighton kwenye mchezo wa FA.


EmoticonEmoticon