Sio Bongo tu kwa mambo ya kuopoa vi ‘Ben 10’, hata mbele haya mambo yapo. Shemeji wake Kanye West na dada yake Kim Kardashian, Kourtney Kardashian ameonekana akijiachia na dogo dogo baada ya kuachana na baba wa watoto wake, Scott Disick.

Younes Bendjima ndiye ‘beau’ dogo dogo wa mwanadada huyo ambaye watu wamefananisha umri wake na ule wa Justin Bieber. Wawili hao wameonekana wakiwa katika mahusiano ya siri kwa takribani mwezi mmoja , na hatimaye wameonekana kweupeee wakipigwa picha sehemu za wazi.
Kourtney na Younes wameonekana maeneo ya Beverly Hills, Magharibi mwa Hollywood wakiwa wanafanya shopping baada ya kumaliza kupata Lunch ya pamoja.

Mwaka jana mwezi wa kumi, Younes alionekana na Kourtney katika moja ya club za muziki jijini Paris Ufaransa, na kisha kuonekana tena Los Angeles Marekani mara kadhaa wakiwa wote.
EmoticonEmoticon