Rapa Lord Eyez, amewataka vijana kukaa mbali na matumizi ya dawa za kulevya huku akidai mtu akitumia dawa hizo anakuwa kama ana nuksi.

Lord ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Hela Yangu’, amedai dawa za kulevya ni mbaya na zinatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote.
“Madawa yana nuksi utaona mambo yako hayaendi yanasusua tu,” Lord alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV Jumatatu hii “Dawa za kulevya zimekuwa shinda hasa kwa vijana wengi wanateketea. Nawaambia dawa za kulevya hazijaribi, usiguse, usinuse, usitumie dawa za kulevya kwa sababu ni hatari zitakuangamiza,”
Rapa huyo amedai yeye alipambana kwa muda mrefu mpaka akafanikiwa kuacha matumizi ya dawa hizo hatari.
Lord ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Ray C, anadaiwa kuwa ndiye aliyesababisha mrembo huyo kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya
.
.
EmoticonEmoticon