Kila
siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za
Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account
yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza
kuzipata huko.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya November 20 2016 ni hii kutoka gazeti la Tanzania daima yenye kichwa cha habari ‘Serikali yahakiki vyeti vya ndoa’
#TanzaniaDAIMA Serikali yahakiki vyeti vya ndoa kwa watumishi wake madai wamekuwa wakidanganya ili kupata nauli na stahiki zingine za likizo pic.twitter.com/HW06vcsywP— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
Gazeti la
Tanzania Daima lemieripoti kuwa Serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya
ndoa kwa watumishi wa umma. Hatua hiyo ambayo imewashtua watumishi wengi
wa umma, imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa harakati za Serikali ya Rais
John Magufuli kuhakiki watumishi wa umma ili kuondokana na watumishi
hewa.
Wakati
Serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa
watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali
nchini.
Kwa muhibu
wa Gazeti la Tanzania Daima habari ambazo limezipata zinasema kuwa
serikali imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa baadhi ya
watumishi wa umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili
kupata nauli na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.
Habari
zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala
wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao. Mmoja wa
walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia
Tanzania daima kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye
vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.
>>>’Kweli
tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha
vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo
na kesho zoezi hilo linakamilika‘
Alipoulizwa
sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini
anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa
kuomba likizo.
Wakati walimu wa shule za Ilala
wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa, wilaya nyingine za Temeke,
Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa hizo.
Mmoja wa walimu kutoka Manispaa ya Ilala
alisema kuwa uhakiki huo una lengo la kutaka kuchelewesha zaidi malipo
na stahiki za walimu za likizo ambazo hazijalipwa kwa miaka mingi.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania leo November 1 2016
#MWANANCHI Raia wa China wametapeliwa mil 22.8 wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya RC Makonda pic.twitter.com/EP1cI7uHtf— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Wabunge CCM, CHADEMA kwa nyakati tofauti wajifungia na viongozi kupanga mikakati dhidi ya hoja zitakazowasilishwa bungeni pic.twitter.com/X95I4hAkAd— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Baadhi ya wazazi wa wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu wameeleza kuwa hali zao kiuchumi sio nzuri pic.twitter.com/JqydxtnLlD— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Baadhi ya wazazi wa wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu wameeleza kuwa hali zao kiuchumi sio nzuri pic.twitter.com/JqydxtnLlD— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Rais Magufuli afungua ukurasa mpya na kukoleza ushirikiano na Kenya, asema Kenya ni mshirika nambari moja kwa uwekezaji Tanzania pic.twitter.com/9t31q1SrFa— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Upelelezi kesi ya kumtishia bastola trafiki inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkinga, Mkumbo umekamilika, 18 kutoa ushahidi pic.twitter.com/f9AEABbJah— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI DC Ilala, Sophia Mjema amesema leo watafanya operesheni ya kuwaondoa wamachinga kando ya barabara za mabasi yaendayo haraka pic.twitter.com/upnQDwQXon— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE JPM aweka wazi kuwa ana uhusiano mzuri na Rais wa Kenya na kufichua siri kuwa wamekuwa na mawasiliano ya simu mara kwa mara pic.twitter.com/6N9j40iMHv— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE Wabunge hatarini kukosa malazi Dodoma, baada ya wamiliki 73 wa nyumba za kulala wageni kugoma wakipinga tozo kubwa za manispaa pic.twitter.com/njrXH5n6g4— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE Bodi ya mikopo elimu ya juu imetangaza siku 90 kwa waombaji mikopo mwaka 2016/2017 kukata rufaa ikiwa hawakuridhishwa na upangaji pic.twitter.com/Z8xKf0yZBr— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE Machinga Mwanza wamegoma kuhamia maeneo yaliyotengwa kwa madai baadhi yana migogoro na mengine si mazingira rafiki kwa biashara zao pic.twitter.com/MbnLTKmQij— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MTANZANIA Jukwaa la wahariri lamshutumu Mwenyekiti wa kamati, Serukamba kuwa kikwazo ktk kufanikisha Muswada wa sheria ya huduma za habari pic.twitter.com/aYtL7HSx9k— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MTANZANIA Raia watatu wa China wamepandishwa kizimbani Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka mawili likiwamo la kumteka mwenzao pic.twitter.com/HCqpluGPtI— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#TanzaniaDAIMA Jeshi la zimamoto DSM limejikuta ktk mazingira magumu ya kutekeleza majukumu yake kutokana na uhaba wa vitendea kazi pic.twitter.com/gRWvdvo4on— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#TanzaniaDAIMA CWT Misungwi yatangaza maandamano ya amani kushinikiza mkurugenzi, Mwaiteleke aliyewadekisha walimu aondolewe ktk nafasi yake pic.twitter.com/tDYCC1xLoq— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
#MTANZANIA Rais Kenyatta akwepa kuzungumzia kashfa ya ufisadi wa bil 51 ktk wizara ya afya ambako baadhi ya jamaa zake wametajwa kuhusika pic.twitter.com/p6xeorYH6y— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
EmoticonEmoticon